SlideShare a Scribd company logo
1 of 10
Download to read offline
Mwanza Press Club

            MDAHALO WA WADAU WA HABARI KUHUSU KATIBA




                Hali ya sasa kimaadili katika tasnia ya habari
                                     Na

                                   Denis Mpagaze




TR. 14. 1. 2012




Denis Mpagaze (denis_mpagaze@yahoo.com, +255753665484 ) ni mhadhili na mhariri
msaidizi wa jarida la kitaaluma liitwalo African Communication Research katika Chuo Kikuu
cha Mtakatifu Agustino. Pia anafundisha na kufanya utafiti katika mambo ya maadili ya
uandishi wa habari
Utangulizi

Ukweli unabaki palepale kwamba tasnia ya habari ni tasnia yenye umuhimu
sana kuliko tasnia nyingine zote hapa Duniani na Mbinguni. Ni tasnia
ambayo inamchango mkubwa katika kumsaidia mwanadamu kuyatawala
mazingira yake kwa sababu mtu hawezi kupanga mipango pasipokuwa na
habari. Na anayetegemewa kutoa habari makini ni mwandishi wa habari.
Ndiyomaana leo hii wasomi kwa wasiosoma, walimu kwa wanafunzi,
wafanyabiashara kwa wakulima, vijana kwa wazee, wakubwa kwa wadogo,
mapadri kwa masista hutegemea tasnia ya habari kufahamu nini kimejiri
ndani na nje ya nchi yao. Ukitaka kuamini ninachokiongea hapa piga picha
leo hii unaamka asubuhi hakuna gazeti, televisheni na redio. Nini kitatokea?
Patakuwa hapatoshi kama wasemavyo waswahili. Napenda kutumia nukuu
ya mtaalam mmoja kutoka kitivo cha sayansi ya jamii katika chuo kikuu cha
Columbia, bwana Walter Williams katika kuelezea umuhimu wa Tasnia ya
habari:
       Mbinguni hakutakuwa na uhitaji wa mwanasheria au wakili kwa
       sababu huko hakutakuwa na kesi yoyote, wala hakutakuwa na uhitaji
       wa madaktari kwa sababu hakuna kuugua. Pia Mbinguni hakutakuwa
       na polisi wala askari kwa sababu huko ni amani na upendo.
       Hakutakuwa na maafisa uhamiaji kwa sababu watu watakuwa na viza
       za kudumu. Lakini mbinguni kutakuwa na uhitaji wa Mwandishi wa
       habari kwa sababu upande mmoja wa Mbinguni watahitaji kujua nini
       kinaendelea katika upande mwingine wa Dunia1
   1 In heaven there will be no need for lawyers or magistrates, for the people will not be
   involved in any court cases - there will be no need for doctors because the people will
   not be sick. Also, in heaven, there will be no need for policemen because the people will
   be peaceful and orderly. In heaven there will be no need for immigration and customs
   officers because each resident of heaven will have permanent and multiple visas for
   free movement of goods and people. In heaven there will not be any need for the
   politician because there will be no politics…But in heaven there will be need for
   journalists and the press because the people living in the Western part of heaven will
   want to know what happens to their counterparts in the Easter part of heaven. So also
   will the people living in the Southern part of heaven want to know what happens to
   their counterparts in both the North, East or Western parts of heaven.
Pamoja na umuhimu mkubwa wa tasnia ya habaria kwa jamii bado imebaki
kukosa heshima miiongoni mwa wanajamii waliowengi kama ilivyo tasnia
ya sheria na nyinginezo. Kwa kweli ni taaluma ambayo ukijatambulisha kwa
wanajamii leo wataonesha kila aina ya kutokuwa na imani na wewe.
Kunamsemo wa kwamba count your words before journalists. Maana ya
msemo huu ni kwamba unatakiwa kuwaa makini na mwandishi wa habari
kwani anaweza kubadilisha yale uliyoyaongea na kuripoti ya kwake.


Vijana wengi hawanamvuto wa kwenda hata kusomea taaluma hii ya habari
na hata wale wanaoisomea wengi wanaishia kufanya kazi katika tasnia
nyingine. Utafiti uliofanywa kwa mara ya mwisho na profesa wa
mawawasiliano, Robert White ulionesha kwamba wanafunzi waliokuwa
wanafanya vizuri darasani katika uandishi wa habari wameishia kuajiriwa
kama bank tellers. Leo hii wanafunzi wengi katika tasnia hii hawana ndoto
ya kuwa waandishi kabisa, wengi wanafikiria kuwa maafisa uhusiano(Public
Relations Officials).

Kwa nini?
Ni ukweli usiofichika kuwa tasnia ya habari imekuwa ikilaumiwa kwa kila
kitu kibaya kinachotokea katika jamii. Wanasiasa wanalalamika kwamba
waandishi wa habari wanawachafua, kwamaana kwamba wanawaandika
kinyume cha matakwa yao. Vile vile wasamii ndio kabisa kila siku wanalia
na waandishi wa habari kwamba wanawadhalilisha. Serikali ya Tanzania
imefikia hata hatua ya kutumia nguvu ya dora kuwaadhibu waandishi
wanaoonekana kukiuka matakwa ya serikali.
Madhumuni mahsusi ya kazi hii
Sasabasi lengo la kazi hii nikuripoti utafiti mfupi juu hali ya sasa kimaadili
katika tasnia ya habari Tanzania. Kama tunavyofahamu walio wengi maadili
ya uandishi wa habari ni vigezo na mwenendo mzima katika utekelezaji wa
wa kazi ya taaluma ya uandishi wa habari. Mtaalamu wa mambo ya habari
hayati Francis Kasoma anasema kwamba, maadili ya uandishi wa habari
lazima yaambatane na maadili ya jamii husika. Kwa maana hiyo basi katika
nchi zetu za Kiafrika Kasoma anasema maadili yajikite katika Afri-ethics.
Msingi mkubwa wa maadili ya kiafrika ni kumthamini mtu ndani ya jamii (I
am because we are). Tanzania kama moja ya nchi za Afrika hainabudi kuwa
na tasnia ya habari ianayoendeleza mazuri yaliyomo katika jamii.


Kwahiyo mwandishi yeyote atakayekwenda kinyume na maadili ya kiafrika
basi atakuwa amekiuka misingi ya taaluma yake, hivyo ni jukumu la
wanajamii kumkanya na kujirekebisha. Kwa sababu mtu mmoja anauwezo
wa kuchafua familia nzima (SAMAKI MMOJA AKIOZA WOTE WAMEOZA) ni
falsafa ambayo inaongoza maadili ya kiafrika.


Tathmini kutoka kwa mlaji wa habari Tanzania
Kimsingi ili ujue tabia yako unatakiwa kuwauliza wanaokufahamu na siyo
kujiuliza mwenyewe. Leo hii ukimfuata mwandishi yeyote wa habari na
ukamuuliza aseme juu ya maadili ya habari haitakuwa rahisi kukupa ukweli.
Sana atavutia upande wake kwamba anafanya vizuri. Sasa mimi kama
mwanataluma ili kuondoa vionjo vyangu binafsi suala hili niliwaanchia
walaji wa habari wafanye tathmini hii. Kutokana na ufinyu wa muda wa
kuandaa mada hii (nimepewa siku tatu) niliamua kutumia moja ya mitandao
ya kijamii yaani Face Book katika kukusanya maoni ya wanajamii juu ya hali
ya sasa kimaadili katika tasnia ya habari. Ilikuwa rahisi kutumia Face Book
kwa sababu inarahisisha kufahamu nani yuko hewani kwa wakati huo na
kumuomba atoe maoni yake. Mpaka asubuhi ya leo washiriki 55
wamejitokeza katika kutoa maaoni juu ya maadili ya tasnia hii kwa sasa.
Wachangiaji wote wameoneshwa kutofurahishwa na mwenendo mzima wa
vyombo vya habari Tanzania kwa kukiuka maadili yao. Sifaeli E. Muddy
anasema:
     Wengi wa waandaji wa habari,wameingiza hisia binafsi katika
     uandaaji wa vipindi, hasa hasa hisia za ushabiki wa kisiasa.. ikiwepo
     na ushabiki wa wamiliki.. utakuta kama chombo kinamilikiwa na
     serikali ,siku zote habari zitakuwa zinakipamba chama tawala na
     kuficha yale mabaya, mfano mzuri juu ya hilo, ni miezi kadhaa
     iliyopita, chombo kimoja kikubwa cha habari kilimtimua kazi
     mkurugenzi kisa kurusha habari ambazo zinaponda wamiliki wake..
     kwa maana hiyo maadili ya habari yanakiukwa sana ndani ya nchi
     yetu.
Omar Suleiman yeye anasema kwamba maadili yakochini hasa ukizingatia
vyombo vingi vya habari viko kiushabiki, kwa maana ya kwamba kama kuna
kitu au mtu anapendwa na mwandishi au chombo cha habari fulani
ataandikwa au atatangazwa kwa kupambwa hata kama hafanyi mema.


Kwa kawaida maadili katika tasnia hii yanajieleza wazi kwamba mwandishi
hatakiwi kuonesha aina yoyote ya ushabiki wala kuegemea katika upande
wowote.Mwandishi mzuri ni yule asiyeonesha chembe hata moja ya hisia
zake anapokuwa kazini.


Utafiti wangu pia unaonesha jinsi gani wanajamii wamefikia hatua hata ya
kuwanawasiwasi kama kweli Tanzania tunawaandishi wa habari au la.
Bryan Majenga anasema:
      Mie naona hivi kuna waandishi na watangajazi katika taaluma ya
      habari ... Lakini Tanzania kwetu kuna wadaku na wazungumzaji !
news values hazizingatiwi ! Mapresenters badala ya Kupresent wana
     zungumza nonsense.
Hapa Bryan anafahamu kabisa mwandishi bora atajikita katika maadili yake
na anapopotoka anashindwa kuamini kama kweli amepitia taaluma hii ya
uandishi wa habari ingawa kujua sio kutenda. Mtu anaweza kuwa amesoma
vizuri kabisa lakini sababu ya mazingira flani anashindwa kufuata yale
aliyofundishwa.


Kutokana na utendaji kazi usioiridhisha jamii, utafiti wangu anaonesha
kwamba waandishi wa habari kubatizwa majina mengi ya kuudhi kama vile
kanjanja, mdaku, mmbeya, tapeli, muongo na mengine mengi. Fredrick
Stanley anasema: maadili ya vyombo vya habari sio mazuri sana we fikiria
mpaka kuna magazeti yanaitwa ya udaku,unafikiria nini kitachoandwikwa
hapo?.


Utafiti pia unaonesha kwamba tasnia ya habari imekosa dira baada ya kuwa
imeacha kufuata maadili yake. Pius Maro anasema:
      Vyombo vya habari havina dira kwani vinakwenda na
      matukio.Wanatupa kile wanachotaka wao na sicho tunachotaka sisi.
      Hakuna uchambuzi wa kina juu ya uchumi bali vimebaki kuwa
      vyombo vya habari vya matukio. Unaweza kupata kichaa ukiendelea
      kufuatilia vyombo vya habari vya Tanzania.

Mdashiru anasema tatizo la vyombo vyetu vya habari vimekuwa vikilinda
maslahi ya wamiliki badala ya kujikita katika kuisaidia jamii kwa ujumla.


Swali la msingi
Hivi, kunauhalali wowote kwa tasnia ya habari kubeba tuhuma hizo? Kama
jibu ni ndiyo Je, mambo hayo waandishi wa habari wanayafanya kwa
makusudi au ni kutokujua maadaili ya habari? Inafamika kabisa maadili ya
waandishi wa habari ni kutekeleza yale ambayo tasnia yake humtaka
kutekeleza. Kama tunavyojua bila kujali mwandishi anatokea chombo gani,
Duniani pote msingi wa maadili ya uandishi wa habari ni kumsaidia
mwananchi kupata taarifa muhimu ili aweze kuyatawala maisha yake. Sasa
basi mwandishi anapoonekana kushindwa kutekeleza hayo anakuwa
kinyume na taaluma yake na matokeo yake ni kudharauliwa na jamii
inayomzunguka. Kwa mfano unategemea nini pale chombo cha habari
kutetea maslahi ya watu wachache na kusahau ya watu wengi? Mchangiaji
mmoja, David Secha anasema
     vyombo vya habari sasa vimekuwa na tabia ya kuhubiri yale yaliyo
     mazuri hususani mjini na kusahau vijijini ambako asilimia 80 ni
     wakulima duni wasio na jinsi ya kujikwamua kiuchumi.

Prosper Mwitinda anasema waandishi wamekosa ubunifu katika kufanya
kazi yao, na badala yake wanakaa tu mijini wakisubiria wapate habari
badala ya kuzunguka maeneo mbalimbali kutafuta habari ambazo jamii
inatakiwa kupata.


Ni jambo la kushangaza kwa baadhi ya vyombo vya habari kugeuka na
kuwa wasemaji wa wanasiasa wachache tena wale wanaopatikana mijini tu.
Mbaya zaidi ni pale ambapo baadhi ya vyombo vya habari kugeuka na kuwa
uwanja wa mapambano ya wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa. Leo hii
kunamajina ya watu haipiti siku hujayasikia katika vyombo vyetu vya habari
wakioneshwa ubaya wao. Hapa mchangiaji mmoja anasema. “media
nyingine zinaandika habari kwa kuchafua tu bila hoja za msingi”. Prosper
Mwitinda anasema:
     The journalists of nowadays write news which are beneficial to
     particular people or group of people BUT not for the whole majority.
     Utakuta mwandishi anapewa kifuta jasho sisi wasomi tunaita "Brown
     Envelope'' ili andike story fulani kwa ajili ya watu fulani, this is
     UNETHICAL.
Chukizo kwa jamii?
Pengine wananchi wanatuhumu vyombo vya habari kwa kuchafua maadili
ya kitanzania. Kwa mfano ni ukweli usiopingika kwamba hivi karibuni
kunavituo vya redio na television vimekuwa vikitangaza matangazo ya
kikundi   kimoja   cha   taarabu   kijulikanacho   kama   KANGA    MOKO
NDEMBENDEMBE-LAKI SI PESA. Sio utamaduni kabisa wa mtanzania kuvaa
nguo zinazooenesha viungo vya ndani. Utafiti wangu unaonesha watu
hawajafurahishwa kabisa na mwenendo huu na kutupa lawama kwa tasnia
ya habari kwa kueneza utamaduni huu. Neema Emmanuel Sway kuhusu
kikundi hiki anasema:
      Sometimes media ziwe zinachuja vitu vya kupresent kwa audience.
      Leo wadogo zetu wanajifunza nini kwao? Kwani wana tofauti gani na
      wanao cheza uchi? Alafu wanahitaji kuheshimiwa eti wapo kazini nani
      atakueshimu ikiwa mwenyewe haujieshimu? Media hazifikirii watoto
      wanajifunza nini wao wanawaza kupata hela tu..hawatambui kama
      wanaharibu society yao? Ingekuwa amri yangu hawa kanga moko
      ningewafunga miaka 30 kwa kuharibu jamii kwa makusudi. kumbuka
      media zina power zaidi ya kuharibu na kutengeneza zingekuwa zina
      wakritisaizi wasingefika mbali lakini siku hizi kanga moko imekuwa
      slogan Tanzania. Eti laki si pesa kama ingekuwa si pesa wange cheza
      uchi?
Picha tunayoipata hapa ni kwamba baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa
vikihabarisha umma kama vile vyenyewe siyo sehemu ya umma.
Vinashindwa kuelewa leo jamii inapoharibika navyo vitaathirika. Kwa
mfano Kikundi hiki kwa namna moja au nyingine kineweza kuchochea hamu
ya kufanya ngono miongoni mwa wanajamii na watu wengi kuishia
kuathirika na gonjwa la UKIMWI. Sasa basi serikali itajikuta ikitumia pesa
nyingi kwa kuwahudumia waathirika amabazo zingetumika kujenga
barabara. Katika taaluma ya Management tunasema waandishi wa habari
wanaongozwa na kanuni ya WIN-LOSE GAME badala ya WIN-WIN.
Wachangiaji, Bunigini Willy na David Secha wanasema kwamba maadili ya
vyombo vya habari hushuka siku hadi siku kutokana na kuweka masilahi
mbele kuliko utu hii inatokana na vyombo vingi kumilikiwa na tabaka
tawala kwani wao ndio wana amua kipi kisikike na kipi kisisikike.
Deogratias Konyani anasema:
     kwa upande wa maadili, hasa kwa upande wa print media!
     Wanafikiria sana kuuza kuliko uzito wa yale wanayoyatoa kwa jamii
     wakisahau kuwa hata watoto wao wanaathirika na habari hizo
     maarufu kama "udaku" hatukatai, kuburudika kupo lakini si
     kuonyesha kwa picha wazi watu waliofumaniwa, walio kwenye kumbi
     za burudani, fukwe za mahoteli nk. mfano, itaburudisha na kusisimua
     kwa wapenda udaku kuona msanii/kiongozi au mtu maarufu
     kafumaniwa gest na mke wa mtu tena na picha wazi zikiwaonesha
     wapo kwenye mikao ya aibu lakini ki mantiki haijengi na ukizingatia
     ni nchi yenye matatizo lukuki ya kuzungumziwa!

Kinachowashangaza zaidi wanajamii ni pale ambapo hata chombo cha
habari cha Taifa kinapokuwa katika mrorongo wa kuharibu maadili ya jamii.
Yacny Senge anasema: Leo hii hata TBC1 wanarusha sebene linaloonesha
mdada akidansi nusu uchi mchana tunakula...! Tv ya taifa haichuji maadili?
Bwana Fredrick Stanley anasema: kuna television nyingine zinaonesha
movie au miziki ambayo kama umekaa na wazazi wako au dada zako
utaondoka mwenyewe. Sio utamaduni wetu bwana lazima tutunze
utamaduni wetu.


Hitimisho
Pamoja na utafiti wangu kuonesha kwamba hali ya maadili ya sasa katika
tasnia ya habari hairidhishi bado nabaki kuamini kwamba maadili ya
uandishi kwa sasa ni mazuri isipokuwa wapo waandishi wachache tena sana
tu wanaoipaka matope tasnia hii. Hili halikwepeki kwani falsafa yetu ya
watu wa Afrika tunaamini kabisa SAMAKI MMOJA AKIOZA WOTE
WAMEOZA. Ndiyomaana hata katika familia zetu mtu mmoja akifanya
mambo ya aibu katika jamii familia yote itachafuka. Sasa basi tasnia ya
habari kama familia tunatakiwa tuwe kitu kimoja, tupendane na tuhakikishe
pale mwenzetu anapokosea tunarekebisha. Kwa kufanya hivyo tutarejesha
heshima ya taaluma yetu ya habari kwa jamii.
              Rafiki mzuri ni akuoneshaye mapungufu yako


                           Asnteni kunisikiliza

More Related Content

Viewers also liked

CodersTrust Bangladesh Student Fund 1-09-2015
CodersTrust Bangladesh Student Fund 1-09-2015CodersTrust Bangladesh Student Fund 1-09-2015
CodersTrust Bangladesh Student Fund 1-09-2015Ferdinand Kjærulff
 
Alt solunum yolu enfeksi̇yonlarinda opti̇mal örnek alim yerleri̇
Alt solunum yolu enfeksi̇yonlarinda  opti̇mal örnek alim yerleri̇Alt solunum yolu enfeksi̇yonlarinda  opti̇mal örnek alim yerleri̇
Alt solunum yolu enfeksi̇yonlarinda opti̇mal örnek alim yerleri̇edoktor
 
Ctrmc answers to osha nprm questions 7 10 final
Ctrmc answers to osha nprm questions 7 10 finalCtrmc answers to osha nprm questions 7 10 final
Ctrmc answers to osha nprm questions 7 10 finalDaddy DeVinney
 
Narciso.it il bello degli uomini
Narciso.it il bello degli uominiNarciso.it il bello degli uomini
Narciso.it il bello degli uominiciorci
 
Citizen Voices in a Networked Age of #BigData
Citizen Voices in a Networked Age of #BigDataCitizen Voices in a Networked Age of #BigData
Citizen Voices in a Networked Age of #BigDataStuart Shulman
 
Azterlan gabonak
Azterlan gabonakAzterlan gabonak
Azterlan gabonakAzterlan
 
Somma di due monomi per la loro differenza
Somma di due monomi per la loro differenzaSomma di due monomi per la loro differenza
Somma di due monomi per la loro differenzaAntonino Giardina
 

Viewers also liked (17)

The Coder
The CoderThe Coder
The Coder
 
CodersTrust Bangladesh Student Fund 1-09-2015
CodersTrust Bangladesh Student Fund 1-09-2015CodersTrust Bangladesh Student Fund 1-09-2015
CodersTrust Bangladesh Student Fund 1-09-2015
 
Alt solunum yolu enfeksi̇yonlarinda opti̇mal örnek alim yerleri̇
Alt solunum yolu enfeksi̇yonlarinda  opti̇mal örnek alim yerleri̇Alt solunum yolu enfeksi̇yonlarinda  opti̇mal örnek alim yerleri̇
Alt solunum yolu enfeksi̇yonlarinda opti̇mal örnek alim yerleri̇
 
Love
LoveLove
Love
 
A step towards Maturity...
A step towards Maturity...A step towards Maturity...
A step towards Maturity...
 
Fairtrade quiz
Fairtrade quizFairtrade quiz
Fairtrade quiz
 
Class album
Class albumClass album
Class album
 
Paracetamol
ParacetamolParacetamol
Paracetamol
 
Title V ed code
Title V ed codeTitle V ed code
Title V ed code
 
Ctrmc answers to osha nprm questions 7 10 final
Ctrmc answers to osha nprm questions 7 10 finalCtrmc answers to osha nprm questions 7 10 final
Ctrmc answers to osha nprm questions 7 10 final
 
Narciso.it il bello degli uomini
Narciso.it il bello degli uominiNarciso.it il bello degli uomini
Narciso.it il bello degli uomini
 
Citizen Voices in a Networked Age of #BigData
Citizen Voices in a Networked Age of #BigDataCitizen Voices in a Networked Age of #BigData
Citizen Voices in a Networked Age of #BigData
 
Autism
AutismAutism
Autism
 
Azterlan gabonak
Azterlan gabonakAzterlan gabonak
Azterlan gabonak
 
Comic commands
Comic commandsComic commands
Comic commands
 
Three Disruptions In One
Three Disruptions In OneThree Disruptions In One
Three Disruptions In One
 
Somma di due monomi per la loro differenza
Somma di due monomi per la loro differenzaSomma di due monomi per la loro differenza
Somma di due monomi per la loro differenza
 

More from Denis Mpagaze

Sr. Lekule on "Lekule2The role of Community Radio in Promoting Social Develop...
Sr. Lekule on "Lekule2The role of Community Radio in Promoting Social Develop...Sr. Lekule on "Lekule2The role of Community Radio in Promoting Social Develop...
Sr. Lekule on "Lekule2The role of Community Radio in Promoting Social Develop...Denis Mpagaze
 
Leonidas Irene's on "Final draft pdfThe contribution of advertisement on incr...
Leonidas Irene's on "Final draft pdfThe contribution of advertisement on incr...Leonidas Irene's on "Final draft pdfThe contribution of advertisement on incr...
Leonidas Irene's on "Final draft pdfThe contribution of advertisement on incr...Denis Mpagaze
 
Liembe Ibrahim on, "The Influence of Soap Operas on Youth Moral Behavior in M...
Liembe Ibrahim on, "The Influence of Soap Operas on Youth Moral Behavior in M...Liembe Ibrahim on, "The Influence of Soap Operas on Youth Moral Behavior in M...
Liembe Ibrahim on, "The Influence of Soap Operas on Youth Moral Behavior in M...Denis Mpagaze
 
Fariat Juma's work on, "Ethical Dilemma Facing Public Relations Practitioners...
Fariat Juma's work on, "Ethical Dilemma Facing Public Relations Practitioners...Fariat Juma's work on, "Ethical Dilemma Facing Public Relations Practitioners...
Fariat Juma's work on, "Ethical Dilemma Facing Public Relations Practitioners...Denis Mpagaze
 
Final draft corrected pdf
Final draft corrected pdfFinal draft corrected pdf
Final draft corrected pdfDenis Mpagaze
 
Laurian Victor on , "The Impact of Facebook Usage on SAUT Youth Moral Behavior"
Laurian Victor on , "The Impact of Facebook Usage on SAUT Youth Moral Behavior"Laurian Victor on , "The Impact of Facebook Usage on SAUT Youth Moral Behavior"
Laurian Victor on , "The Impact of Facebook Usage on SAUT Youth Moral Behavior"Denis Mpagaze
 
GIFT MACHA ON, " The Decline of Investigative Journalism in Tanzania: Case St...
GIFT MACHA ON, " The Decline of Investigative Journalism in Tanzania: Case St...GIFT MACHA ON, " The Decline of Investigative Journalism in Tanzania: Case St...
GIFT MACHA ON, " The Decline of Investigative Journalism in Tanzania: Case St...Denis Mpagaze
 
Tanzanian media position in framing crime issues
Tanzanian media position in framing crime issuesTanzanian media position in framing crime issues
Tanzanian media position in framing crime issuesDenis Mpagaze
 
Corruption in the media: Perceptions of Tanzanian journalists
Corruption in the media: Perceptions of Tanzanian journalists Corruption in the media: Perceptions of Tanzanian journalists
Corruption in the media: Perceptions of Tanzanian journalists Denis Mpagaze
 
New Media and Traditional Media
New Media and Traditional MediaNew Media and Traditional Media
New Media and Traditional MediaDenis Mpagaze
 

More from Denis Mpagaze (12)

Sr. Lekule on "Lekule2The role of Community Radio in Promoting Social Develop...
Sr. Lekule on "Lekule2The role of Community Radio in Promoting Social Develop...Sr. Lekule on "Lekule2The role of Community Radio in Promoting Social Develop...
Sr. Lekule on "Lekule2The role of Community Radio in Promoting Social Develop...
 
Sr.lekule final doc
Sr.lekule final docSr.lekule final doc
Sr.lekule final doc
 
Leonidas Irene's on "Final draft pdfThe contribution of advertisement on incr...
Leonidas Irene's on "Final draft pdfThe contribution of advertisement on incr...Leonidas Irene's on "Final draft pdfThe contribution of advertisement on incr...
Leonidas Irene's on "Final draft pdfThe contribution of advertisement on incr...
 
Liembe Ibrahim on, "The Influence of Soap Operas on Youth Moral Behavior in M...
Liembe Ibrahim on, "The Influence of Soap Operas on Youth Moral Behavior in M...Liembe Ibrahim on, "The Influence of Soap Operas on Youth Moral Behavior in M...
Liembe Ibrahim on, "The Influence of Soap Operas on Youth Moral Behavior in M...
 
Fariat Juma's work on, "Ethical Dilemma Facing Public Relations Practitioners...
Fariat Juma's work on, "Ethical Dilemma Facing Public Relations Practitioners...Fariat Juma's work on, "Ethical Dilemma Facing Public Relations Practitioners...
Fariat Juma's work on, "Ethical Dilemma Facing Public Relations Practitioners...
 
Final draft corrected pdf
Final draft corrected pdfFinal draft corrected pdf
Final draft corrected pdf
 
Laurian Victor on , "The Impact of Facebook Usage on SAUT Youth Moral Behavior"
Laurian Victor on , "The Impact of Facebook Usage on SAUT Youth Moral Behavior"Laurian Victor on , "The Impact of Facebook Usage on SAUT Youth Moral Behavior"
Laurian Victor on , "The Impact of Facebook Usage on SAUT Youth Moral Behavior"
 
GIFT MACHA ON, " The Decline of Investigative Journalism in Tanzania: Case St...
GIFT MACHA ON, " The Decline of Investigative Journalism in Tanzania: Case St...GIFT MACHA ON, " The Decline of Investigative Journalism in Tanzania: Case St...
GIFT MACHA ON, " The Decline of Investigative Journalism in Tanzania: Case St...
 
Tanzanian media position in framing crime issues
Tanzanian media position in framing crime issuesTanzanian media position in framing crime issues
Tanzanian media position in framing crime issues
 
Corruption in the media: Perceptions of Tanzanian journalists
Corruption in the media: Perceptions of Tanzanian journalists Corruption in the media: Perceptions of Tanzanian journalists
Corruption in the media: Perceptions of Tanzanian journalists
 
Corruption
CorruptionCorruption
Corruption
 
New Media and Traditional Media
New Media and Traditional MediaNew Media and Traditional Media
New Media and Traditional Media
 

Kongamano

  • 1. Mwanza Press Club MDAHALO WA WADAU WA HABARI KUHUSU KATIBA Hali ya sasa kimaadili katika tasnia ya habari Na Denis Mpagaze TR. 14. 1. 2012 Denis Mpagaze (denis_mpagaze@yahoo.com, +255753665484 ) ni mhadhili na mhariri msaidizi wa jarida la kitaaluma liitwalo African Communication Research katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino. Pia anafundisha na kufanya utafiti katika mambo ya maadili ya uandishi wa habari
  • 2. Utangulizi Ukweli unabaki palepale kwamba tasnia ya habari ni tasnia yenye umuhimu sana kuliko tasnia nyingine zote hapa Duniani na Mbinguni. Ni tasnia ambayo inamchango mkubwa katika kumsaidia mwanadamu kuyatawala mazingira yake kwa sababu mtu hawezi kupanga mipango pasipokuwa na habari. Na anayetegemewa kutoa habari makini ni mwandishi wa habari. Ndiyomaana leo hii wasomi kwa wasiosoma, walimu kwa wanafunzi, wafanyabiashara kwa wakulima, vijana kwa wazee, wakubwa kwa wadogo, mapadri kwa masista hutegemea tasnia ya habari kufahamu nini kimejiri ndani na nje ya nchi yao. Ukitaka kuamini ninachokiongea hapa piga picha leo hii unaamka asubuhi hakuna gazeti, televisheni na redio. Nini kitatokea? Patakuwa hapatoshi kama wasemavyo waswahili. Napenda kutumia nukuu ya mtaalam mmoja kutoka kitivo cha sayansi ya jamii katika chuo kikuu cha Columbia, bwana Walter Williams katika kuelezea umuhimu wa Tasnia ya habari: Mbinguni hakutakuwa na uhitaji wa mwanasheria au wakili kwa sababu huko hakutakuwa na kesi yoyote, wala hakutakuwa na uhitaji wa madaktari kwa sababu hakuna kuugua. Pia Mbinguni hakutakuwa na polisi wala askari kwa sababu huko ni amani na upendo. Hakutakuwa na maafisa uhamiaji kwa sababu watu watakuwa na viza za kudumu. Lakini mbinguni kutakuwa na uhitaji wa Mwandishi wa habari kwa sababu upande mmoja wa Mbinguni watahitaji kujua nini kinaendelea katika upande mwingine wa Dunia1 1 In heaven there will be no need for lawyers or magistrates, for the people will not be involved in any court cases - there will be no need for doctors because the people will not be sick. Also, in heaven, there will be no need for policemen because the people will be peaceful and orderly. In heaven there will be no need for immigration and customs officers because each resident of heaven will have permanent and multiple visas for free movement of goods and people. In heaven there will not be any need for the politician because there will be no politics…But in heaven there will be need for journalists and the press because the people living in the Western part of heaven will want to know what happens to their counterparts in the Easter part of heaven. So also will the people living in the Southern part of heaven want to know what happens to their counterparts in both the North, East or Western parts of heaven.
  • 3. Pamoja na umuhimu mkubwa wa tasnia ya habaria kwa jamii bado imebaki kukosa heshima miiongoni mwa wanajamii waliowengi kama ilivyo tasnia ya sheria na nyinginezo. Kwa kweli ni taaluma ambayo ukijatambulisha kwa wanajamii leo wataonesha kila aina ya kutokuwa na imani na wewe. Kunamsemo wa kwamba count your words before journalists. Maana ya msemo huu ni kwamba unatakiwa kuwaa makini na mwandishi wa habari kwani anaweza kubadilisha yale uliyoyaongea na kuripoti ya kwake. Vijana wengi hawanamvuto wa kwenda hata kusomea taaluma hii ya habari na hata wale wanaoisomea wengi wanaishia kufanya kazi katika tasnia nyingine. Utafiti uliofanywa kwa mara ya mwisho na profesa wa mawawasiliano, Robert White ulionesha kwamba wanafunzi waliokuwa wanafanya vizuri darasani katika uandishi wa habari wameishia kuajiriwa kama bank tellers. Leo hii wanafunzi wengi katika tasnia hii hawana ndoto ya kuwa waandishi kabisa, wengi wanafikiria kuwa maafisa uhusiano(Public Relations Officials). Kwa nini? Ni ukweli usiofichika kuwa tasnia ya habari imekuwa ikilaumiwa kwa kila kitu kibaya kinachotokea katika jamii. Wanasiasa wanalalamika kwamba waandishi wa habari wanawachafua, kwamaana kwamba wanawaandika kinyume cha matakwa yao. Vile vile wasamii ndio kabisa kila siku wanalia na waandishi wa habari kwamba wanawadhalilisha. Serikali ya Tanzania imefikia hata hatua ya kutumia nguvu ya dora kuwaadhibu waandishi wanaoonekana kukiuka matakwa ya serikali.
  • 4. Madhumuni mahsusi ya kazi hii Sasabasi lengo la kazi hii nikuripoti utafiti mfupi juu hali ya sasa kimaadili katika tasnia ya habari Tanzania. Kama tunavyofahamu walio wengi maadili ya uandishi wa habari ni vigezo na mwenendo mzima katika utekelezaji wa wa kazi ya taaluma ya uandishi wa habari. Mtaalamu wa mambo ya habari hayati Francis Kasoma anasema kwamba, maadili ya uandishi wa habari lazima yaambatane na maadili ya jamii husika. Kwa maana hiyo basi katika nchi zetu za Kiafrika Kasoma anasema maadili yajikite katika Afri-ethics. Msingi mkubwa wa maadili ya kiafrika ni kumthamini mtu ndani ya jamii (I am because we are). Tanzania kama moja ya nchi za Afrika hainabudi kuwa na tasnia ya habari ianayoendeleza mazuri yaliyomo katika jamii. Kwahiyo mwandishi yeyote atakayekwenda kinyume na maadili ya kiafrika basi atakuwa amekiuka misingi ya taaluma yake, hivyo ni jukumu la wanajamii kumkanya na kujirekebisha. Kwa sababu mtu mmoja anauwezo wa kuchafua familia nzima (SAMAKI MMOJA AKIOZA WOTE WAMEOZA) ni falsafa ambayo inaongoza maadili ya kiafrika. Tathmini kutoka kwa mlaji wa habari Tanzania Kimsingi ili ujue tabia yako unatakiwa kuwauliza wanaokufahamu na siyo kujiuliza mwenyewe. Leo hii ukimfuata mwandishi yeyote wa habari na ukamuuliza aseme juu ya maadili ya habari haitakuwa rahisi kukupa ukweli. Sana atavutia upande wake kwamba anafanya vizuri. Sasa mimi kama mwanataluma ili kuondoa vionjo vyangu binafsi suala hili niliwaanchia walaji wa habari wafanye tathmini hii. Kutokana na ufinyu wa muda wa kuandaa mada hii (nimepewa siku tatu) niliamua kutumia moja ya mitandao ya kijamii yaani Face Book katika kukusanya maoni ya wanajamii juu ya hali
  • 5. ya sasa kimaadili katika tasnia ya habari. Ilikuwa rahisi kutumia Face Book kwa sababu inarahisisha kufahamu nani yuko hewani kwa wakati huo na kumuomba atoe maoni yake. Mpaka asubuhi ya leo washiriki 55 wamejitokeza katika kutoa maaoni juu ya maadili ya tasnia hii kwa sasa. Wachangiaji wote wameoneshwa kutofurahishwa na mwenendo mzima wa vyombo vya habari Tanzania kwa kukiuka maadili yao. Sifaeli E. Muddy anasema: Wengi wa waandaji wa habari,wameingiza hisia binafsi katika uandaaji wa vipindi, hasa hasa hisia za ushabiki wa kisiasa.. ikiwepo na ushabiki wa wamiliki.. utakuta kama chombo kinamilikiwa na serikali ,siku zote habari zitakuwa zinakipamba chama tawala na kuficha yale mabaya, mfano mzuri juu ya hilo, ni miezi kadhaa iliyopita, chombo kimoja kikubwa cha habari kilimtimua kazi mkurugenzi kisa kurusha habari ambazo zinaponda wamiliki wake.. kwa maana hiyo maadili ya habari yanakiukwa sana ndani ya nchi yetu. Omar Suleiman yeye anasema kwamba maadili yakochini hasa ukizingatia vyombo vingi vya habari viko kiushabiki, kwa maana ya kwamba kama kuna kitu au mtu anapendwa na mwandishi au chombo cha habari fulani ataandikwa au atatangazwa kwa kupambwa hata kama hafanyi mema. Kwa kawaida maadili katika tasnia hii yanajieleza wazi kwamba mwandishi hatakiwi kuonesha aina yoyote ya ushabiki wala kuegemea katika upande wowote.Mwandishi mzuri ni yule asiyeonesha chembe hata moja ya hisia zake anapokuwa kazini. Utafiti wangu pia unaonesha jinsi gani wanajamii wamefikia hatua hata ya kuwanawasiwasi kama kweli Tanzania tunawaandishi wa habari au la. Bryan Majenga anasema: Mie naona hivi kuna waandishi na watangajazi katika taaluma ya habari ... Lakini Tanzania kwetu kuna wadaku na wazungumzaji !
  • 6. news values hazizingatiwi ! Mapresenters badala ya Kupresent wana zungumza nonsense. Hapa Bryan anafahamu kabisa mwandishi bora atajikita katika maadili yake na anapopotoka anashindwa kuamini kama kweli amepitia taaluma hii ya uandishi wa habari ingawa kujua sio kutenda. Mtu anaweza kuwa amesoma vizuri kabisa lakini sababu ya mazingira flani anashindwa kufuata yale aliyofundishwa. Kutokana na utendaji kazi usioiridhisha jamii, utafiti wangu anaonesha kwamba waandishi wa habari kubatizwa majina mengi ya kuudhi kama vile kanjanja, mdaku, mmbeya, tapeli, muongo na mengine mengi. Fredrick Stanley anasema: maadili ya vyombo vya habari sio mazuri sana we fikiria mpaka kuna magazeti yanaitwa ya udaku,unafikiria nini kitachoandwikwa hapo?. Utafiti pia unaonesha kwamba tasnia ya habari imekosa dira baada ya kuwa imeacha kufuata maadili yake. Pius Maro anasema: Vyombo vya habari havina dira kwani vinakwenda na matukio.Wanatupa kile wanachotaka wao na sicho tunachotaka sisi. Hakuna uchambuzi wa kina juu ya uchumi bali vimebaki kuwa vyombo vya habari vya matukio. Unaweza kupata kichaa ukiendelea kufuatilia vyombo vya habari vya Tanzania. Mdashiru anasema tatizo la vyombo vyetu vya habari vimekuwa vikilinda maslahi ya wamiliki badala ya kujikita katika kuisaidia jamii kwa ujumla. Swali la msingi Hivi, kunauhalali wowote kwa tasnia ya habari kubeba tuhuma hizo? Kama jibu ni ndiyo Je, mambo hayo waandishi wa habari wanayafanya kwa makusudi au ni kutokujua maadaili ya habari? Inafamika kabisa maadili ya waandishi wa habari ni kutekeleza yale ambayo tasnia yake humtaka
  • 7. kutekeleza. Kama tunavyojua bila kujali mwandishi anatokea chombo gani, Duniani pote msingi wa maadili ya uandishi wa habari ni kumsaidia mwananchi kupata taarifa muhimu ili aweze kuyatawala maisha yake. Sasa basi mwandishi anapoonekana kushindwa kutekeleza hayo anakuwa kinyume na taaluma yake na matokeo yake ni kudharauliwa na jamii inayomzunguka. Kwa mfano unategemea nini pale chombo cha habari kutetea maslahi ya watu wachache na kusahau ya watu wengi? Mchangiaji mmoja, David Secha anasema vyombo vya habari sasa vimekuwa na tabia ya kuhubiri yale yaliyo mazuri hususani mjini na kusahau vijijini ambako asilimia 80 ni wakulima duni wasio na jinsi ya kujikwamua kiuchumi. Prosper Mwitinda anasema waandishi wamekosa ubunifu katika kufanya kazi yao, na badala yake wanakaa tu mijini wakisubiria wapate habari badala ya kuzunguka maeneo mbalimbali kutafuta habari ambazo jamii inatakiwa kupata. Ni jambo la kushangaza kwa baadhi ya vyombo vya habari kugeuka na kuwa wasemaji wa wanasiasa wachache tena wale wanaopatikana mijini tu. Mbaya zaidi ni pale ambapo baadhi ya vyombo vya habari kugeuka na kuwa uwanja wa mapambano ya wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa. Leo hii kunamajina ya watu haipiti siku hujayasikia katika vyombo vyetu vya habari wakioneshwa ubaya wao. Hapa mchangiaji mmoja anasema. “media nyingine zinaandika habari kwa kuchafua tu bila hoja za msingi”. Prosper Mwitinda anasema: The journalists of nowadays write news which are beneficial to particular people or group of people BUT not for the whole majority. Utakuta mwandishi anapewa kifuta jasho sisi wasomi tunaita "Brown Envelope'' ili andike story fulani kwa ajili ya watu fulani, this is UNETHICAL.
  • 8. Chukizo kwa jamii? Pengine wananchi wanatuhumu vyombo vya habari kwa kuchafua maadili ya kitanzania. Kwa mfano ni ukweli usiopingika kwamba hivi karibuni kunavituo vya redio na television vimekuwa vikitangaza matangazo ya kikundi kimoja cha taarabu kijulikanacho kama KANGA MOKO NDEMBENDEMBE-LAKI SI PESA. Sio utamaduni kabisa wa mtanzania kuvaa nguo zinazooenesha viungo vya ndani. Utafiti wangu unaonesha watu hawajafurahishwa kabisa na mwenendo huu na kutupa lawama kwa tasnia ya habari kwa kueneza utamaduni huu. Neema Emmanuel Sway kuhusu kikundi hiki anasema: Sometimes media ziwe zinachuja vitu vya kupresent kwa audience. Leo wadogo zetu wanajifunza nini kwao? Kwani wana tofauti gani na wanao cheza uchi? Alafu wanahitaji kuheshimiwa eti wapo kazini nani atakueshimu ikiwa mwenyewe haujieshimu? Media hazifikirii watoto wanajifunza nini wao wanawaza kupata hela tu..hawatambui kama wanaharibu society yao? Ingekuwa amri yangu hawa kanga moko ningewafunga miaka 30 kwa kuharibu jamii kwa makusudi. kumbuka media zina power zaidi ya kuharibu na kutengeneza zingekuwa zina wakritisaizi wasingefika mbali lakini siku hizi kanga moko imekuwa slogan Tanzania. Eti laki si pesa kama ingekuwa si pesa wange cheza uchi? Picha tunayoipata hapa ni kwamba baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikihabarisha umma kama vile vyenyewe siyo sehemu ya umma. Vinashindwa kuelewa leo jamii inapoharibika navyo vitaathirika. Kwa mfano Kikundi hiki kwa namna moja au nyingine kineweza kuchochea hamu ya kufanya ngono miongoni mwa wanajamii na watu wengi kuishia kuathirika na gonjwa la UKIMWI. Sasa basi serikali itajikuta ikitumia pesa nyingi kwa kuwahudumia waathirika amabazo zingetumika kujenga barabara. Katika taaluma ya Management tunasema waandishi wa habari wanaongozwa na kanuni ya WIN-LOSE GAME badala ya WIN-WIN.
  • 9. Wachangiaji, Bunigini Willy na David Secha wanasema kwamba maadili ya vyombo vya habari hushuka siku hadi siku kutokana na kuweka masilahi mbele kuliko utu hii inatokana na vyombo vingi kumilikiwa na tabaka tawala kwani wao ndio wana amua kipi kisikike na kipi kisisikike. Deogratias Konyani anasema: kwa upande wa maadili, hasa kwa upande wa print media! Wanafikiria sana kuuza kuliko uzito wa yale wanayoyatoa kwa jamii wakisahau kuwa hata watoto wao wanaathirika na habari hizo maarufu kama "udaku" hatukatai, kuburudika kupo lakini si kuonyesha kwa picha wazi watu waliofumaniwa, walio kwenye kumbi za burudani, fukwe za mahoteli nk. mfano, itaburudisha na kusisimua kwa wapenda udaku kuona msanii/kiongozi au mtu maarufu kafumaniwa gest na mke wa mtu tena na picha wazi zikiwaonesha wapo kwenye mikao ya aibu lakini ki mantiki haijengi na ukizingatia ni nchi yenye matatizo lukuki ya kuzungumziwa! Kinachowashangaza zaidi wanajamii ni pale ambapo hata chombo cha habari cha Taifa kinapokuwa katika mrorongo wa kuharibu maadili ya jamii. Yacny Senge anasema: Leo hii hata TBC1 wanarusha sebene linaloonesha mdada akidansi nusu uchi mchana tunakula...! Tv ya taifa haichuji maadili? Bwana Fredrick Stanley anasema: kuna television nyingine zinaonesha movie au miziki ambayo kama umekaa na wazazi wako au dada zako utaondoka mwenyewe. Sio utamaduni wetu bwana lazima tutunze utamaduni wetu. Hitimisho Pamoja na utafiti wangu kuonesha kwamba hali ya maadili ya sasa katika tasnia ya habari hairidhishi bado nabaki kuamini kwamba maadili ya uandishi kwa sasa ni mazuri isipokuwa wapo waandishi wachache tena sana tu wanaoipaka matope tasnia hii. Hili halikwepeki kwani falsafa yetu ya watu wa Afrika tunaamini kabisa SAMAKI MMOJA AKIOZA WOTE WAMEOZA. Ndiyomaana hata katika familia zetu mtu mmoja akifanya
  • 10. mambo ya aibu katika jamii familia yote itachafuka. Sasa basi tasnia ya habari kama familia tunatakiwa tuwe kitu kimoja, tupendane na tuhakikishe pale mwenzetu anapokosea tunarekebisha. Kwa kufanya hivyo tutarejesha heshima ya taaluma yetu ya habari kwa jamii. Rafiki mzuri ni akuoneshaye mapungufu yako Asnteni kunisikiliza