Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Ujiji
1. Ni katika eneo hilo la Ujiji ndiko mvumbuzi wa kimataifa, Dr David Livingstone,
alipofikia akiwa katika safari zake zilizomtoa pwani ya Afrika mashariki hadi Kongo.
Kwa sasa kuna makumbusho maalum kwa heshima yake na kumbu kumbu ya vizazi
vijavyo.
Lakini nusu karne baada ya uhuru wa Tanzania, umaarufu wa mji huo mkongwe
umeporomoka na hali ya maisha ya watu wake imeendelea kuwa duni. Mwandishi wa
BBC Baruan Muhuza ametembelea mji huo na kujionea hali ilivyo.
Kwenye kituo cha makumbusho ya Dr David Livingstone katika eneo la Mnazi Mmoja-
Kabondo Ujiji ni eneo ambalo kuna majengo mazuri yenye vyumba kadhaa vilivyobeba
alama za ujio wa Mvumbuzi huyo aliyechangia kukomeshwa kwa biashara ya utumwa,
lakini pia kumbukumbu za asili za vitu na watu wa mji huo.
Kufifia kwa umaarufu wa eneo kongwe la Ujiji kulichangiwa na sababu nyingi, ikiwemo
kuanzishwa kwa mji mpya wa Kigoma. Kurejea kwa Ndiyunze Msherwampamba
aliyekuwa kiongozi wa watu wa kabila la wagoma kutoka Kongo kuliibua jina la mji
mpya Kigoma.
Alhaj Mikdad bin Ibrahim Tawfiq Malilo mwenye miaka 79 mkaazi maarufu wa Ujiji,
ameiambia BBC kuwa Msherwampamba alipokelewa pamoja na wafuasi wa kabila lake
na wakapewa eneo la kujitawala ambalo wakati huo lilikuwa likiitwa Rusambo , na sasa
ndilo linaloitwa Kigoma.
Miti ya miembe iliyokuwa njia ya watumwa kutoka Ujiji kwenda Bagamoyo
„Walipompokea Msherwampamba wakapewa kanchi, eneo lenyewe ni sehemu hivi sasa
wanasema ikulu ndogo zamani tulikuwa tunasema Kaizahofu, eneo lote lile kabla ya
hapo lilikuwa linaitwa Rusambo.
Sasa wenyeji warundi ndiyo wanajiita wajiji wakawa wanakwenda kuwatembelea
wanasema 'tugende kubagoma,' likaendelea likabadilika ndiyo ikawa Kigoma basi ndiyo
kitovu cha mahala kuitwa Kigoma asili Rusambo”
Kwa miaka mingi nguvu za kiuchumi za wakazi wa mji huo imekuwa ikitegemea Ziwa
Tanganyika kwa uvuvi na usafiri wa kwenda na kutoka maeneo mbali mbali ya
2. mwambao wa ziwa hilo zikiwemo nchi jirani za Burundi, Zambia na Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Kongo.
Pamoja na kupoteza uimara wake, Mji wa Ujiji na Kigoma kwa ujumla umeibuka upya
katika miaka ya karibuni kwa kutoa watu waliojipatia umaarufu mkubwa katika eneo lote
la Afrika Mashariki na kati ikiwa ni pamoja na wasanii wa muziki wakiwemo Naseeb
Abdul anaejulikana zaidi kama Diamond, Wanasoka wastaafu Kitwana Manara, Kassim
Manara, Edibily Lunyamila na hata nahodha wa sasa wa Timu ya Taifa ya Tanzania
Juma Kaseja .
Tangu enzi za Ukoloni watu kutoka maeneo mbalimbali ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya
Kongo, Burundi, Rwanda na Zambia waliingia mji wa Ujiji hasa kipindi cha utawala wa
biashara ya watumwa.
Taarifa zinazohusiana
Tanzania
4.
Habari Muhimu
RSS
Wanawake 60 wakwepa Boko Haram
5. Picha za video na kesi ya Pistorius
Wapiganaji wa kipalestina wauawa Gaza
Picha
Ebola ni janga Afrika
Magharibi
Hapa ndipo homa kali ya Ebola ilipowafikisha wakazi wa mataifa ya Afrika
Magharibi
1.
2.
3.
4.
5.
6.
7.
8.
Mitandao ya Kijamii
1. Kwenye Facebook
Like
2. Kwenye Twitter
Fuata